MWENYEKITI wa Halmashauri ya Wilaya ya Igunga mkoani Tabora,
Onesmo Maluda, amekamatwa na Jeshi la Polisi na kuswekwa ndani kwa tuhuma za
ubadhirifu wa Sh. milioni 35
Agizo la kukamatwa kwa mwenyekiti huo ambaye pia ni diwani
wa Kata ya Choma, lilitolewa hivi karibuni na Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa,
alipokuwa akizungumza na wananchi kwenye mkutano wa hadhara katika Kata
ya Choma hivi karibuni
Aliagiza kukamatwa kwa viongozi wote wanaotuhumiwa kwa
upotevu wa Sh. milioni 35 zilizotolewa na halmashauri ya wilaya hiyo kwa ajili
ya ununuzi wa mashine ya kukoboa mpunga ya Kijiji cha Choma
Majaliwa alieleza kuwa mashine hiyo licha ya kununuliwa,
ilifanya kazi kwa muda mfupi sana ikaharibika, hali iliyoleta sintofahamu kwa
wananchi kutokana na baadhi ya viongozi kulalamikiwa kununua mashine mbovu
Waziri Mkuu alisema licha ya kulalamikiwa kwa ubovu, hata
matengenezo yalishindikana
Akitoa taarifa baada ya kukamatwa kwa mwenyekiti huyo, Mkuu
wa Polisi wilayani humo, Ally Mkalipa, alisema mwenyekiti huyo alikamatwa na
kuunganishwa na watuhumiwa wenzake wanane kwa tuhuma za kuhusika na upotevu wa
fedha hizo
Alisema polisi wanaendelea kuwatafuta watuhumiwa wengine
akiwamo mkandarasi, Sadick Hans, ambaye alitoroka baada ya kusikia anatafutwa
Agizo la JPM lamuingiza Mwenyekiti matatani.
Reviewed by KUSAGANEWS
on
August 23, 2018
Rating:

No comments:
Post a Comment