Serikali imetangaza kuondoa mamlaka ya baraza ka madiwani
kupendekeza kufutwa kazi kwa wataalamu wa ardhi kuanzia Julai Mosi
Msimamo huo umetolewa na Waziri wa Ardhi, Nyumba na
Maendeleo ya Makazi, William Lukuvi leo, Julai 13 alipokutana na kampuni
binafsi za upangaji na upimaji miji, watendaji wa mitaa na vijiji
Waziri ametoa msimamo huo akisema mkakati huo unakusudia
kuwapa maofisa ardhi wa halmashauri uhuru wa kutekeleza majukumu yao bila
kuingiliwa na madiwani
"Diwani akikuambia upime eneo la wazi kataa. Hawezi
kukufukuza. Ukiteleza ukakosea kuutumia uhuru wako, utafukuzwa kazi wewe mwenyewe,"
amesema Lukuvi
Akieleza umuhimu wa uamuzi huo, waziri amesema utaondoa
ujenzi na uvamizi unaofanywa maeneo ya wazi kwa shinikizo kutoka kwa madiwani
hivyo kuongeza makazi holela maeneo mengi ya mjini.
Kurahisisha upimaji,
urasmishaji wa makazi holela ambako wananchi wengi wa kipato cha chini
wanaishi, amesema Serikali imefungua ofisi katika kanda nane ambako masuala
yote ya ardhi yatashughulikiwa
"Kuanzia sasa, mtakuja wizarani kutusalimia tu. Mambo
yote mtayamaliza kwenye ofisi za kanda ambako maofisa wote watakuwapo,"
amesema
Amezitaja ofisi hizo za kanda kuwa ni Dar es Salaam, Dodoma,
Moshi, Simiyu, Mwanza, Mtwara, Tabora na Mbeya
Mabaraza ya madiwani hayana mamlaka kumfutakazi mtaalam wa ardhi
Reviewed by KUSAGANEWS
on
July 13, 2018
Rating:
No comments:
Post a Comment