Waziri wa
Mambo ya Ndani, Kangi Lugola amemhakikishia Rais John Magufuli kuwa atapambana
na ajali za barabarani na kwamba zitapungua na kwisha kabisa ndani ya muda
mfupi ujao
Siku chache
zilizopita wakati wa kuwaapisha mawaziri pamoja na viongozi mbalimbali
aliowateua Magufuli alisema amechoka kutoa rambirambi kutokana na mfululizo wa
ajali za barabaran hususani Mkoa wa Mbeya
Lugola amesema
hayo leo Julai 14 wakati Rais akimuapisha Kamishna Jenerali wa Jeshi la
magereza Phaustine Kasike na Naibu Katibu Mkuu Ofisi ya Makamu wa Rais na
Muungano Joseph Sokoine viwanja vya Ikulu jijini Dar es Salaam.
“Ulivyoniapisha
yapo mambo ya msingi ambayo ulinielekeza niyafanyie kazi nataka nikuhakikishie
mambo hayo nimeshaanza kuyafanyia kazi, pamoja na makatibu wangu,”amesema na
kuongeza kuwa
“Ili kuonyesha
kwamba tumeyapa uzito na kuanza kuyatekeleza pasipo mzaha tayari kwenye upande
wa ajali tumeshaanza kuchukua hatua na nataka nikuthibitishie kwamba utapata
usingizi na hata salamu za pole zitapungua na zitakwenda kwisha kabisa ndani ya
muda mfupi ujao.”
Kingine
alizungumzia kuhusu mikataba ya hovyo ya kifisadi na kulidhalilisha taifa
“Hatuwezi kuwa
na tuhuma za Watanzania zisizoisha na kuleta sintofahamu, vitendo hivi
lazima vifike mwisho, hivyo nakuahidi kwa kuwa umeniamini na mimi nitafanya
kazi bila kujali nafasi ya mtu wala upendeleo,”amesema
Lugola amhakikishia Rais Magufuli atazimaliza ajali za barabarani
Reviewed by KUSAGANEWS
on
July 14, 2018
Rating:
No comments:
Post a Comment