Giza la sintofahamu ladaiwa
kutanda Mkoa wa Iringa, ikiwa ni baada ya mgombea wa udiwani kwa tiketi
ya CHADEMA kutojulikana alipo baada ya kuchukuliwa na na watu
wasiojulikana mapema ya leo.
Akizungumza
kuhusu sintofahamu hiyo kwa njia ya simu, Mbunge wa Iringa Mjini,
Mchungaji Peter Msigwa amesema kwamba sintofahamu hiyo ilianza
kujitokeza siku ya juzi baada ya aliyekuwa mgombea wa Kata ya Kwakilosa
kunyang'anywa fomu na mtu aliyemuonyesha bastola hali iliyomuingiza woga
mgombea Godfrey Luchagile na kumfanya ajitoe katika kinyang'anyiro
hicho.
"Hii ilianza juzi baada ya Mgombea Godfrey Luchagile, kudai kutishwa na bastola kisha kunyang'anywa fomu ya uchaguzi, baadaye mgombea aliyepatikana kuziba nafasi yake ndg. Hamid Mfalingungi naye kapotea mapema ya leo, huyu wa Galilonga yeye alinyang'anywa fomu lakini bahati nzuri alikuwa ameshaitoa 'photocopy' wakati anairudisha anaambiwa kagushi hivyo wamempeleka polisi ili kupoteza muda wa kupokea fopmu. Hatujui nia yao kwani katika Kata tatu tumemaliza zoezi hili salama ila hizi mbili ndiyo mambo haya yanaibuka,"
Akizungumzia kwa undani kuhusu tukio hilo, Katibu wa CHADEMA mkoani Iringa Jackson Mnyamwani amesema kuwa wakati sinema hiyo inaendelea Msimamizi Msaidizi wa Uchaguzi, kata ya Kwakilosa, Ndg. Fuad Mwakitosa amegoma kupokea fomu ya mgombea ambaye ilirudishwa na wadhamini wake kitu ambacho ni kinyume na utaratibu.
Pamoja na hayo, Mch Peter Msigwa amesema kwamba tayari siku ya jana walikwisha wasiliana na Mkurugenzi wa Uchaguzi Taifa Athuman Kihamia kwa ajili ya sintofahamu hiyo lakini mpaka sasa hakuna kitu kinachoonekana kuendelea.
Uchaguzi wa marudio unatarajiwa
kufanyika Agosti 12, 2018, katika jimbo la Buyungu, Kigoma na kata 77
baada ya madiwani wengi kuhama vyama vya upinzani na kuhamia CCM wakidai
wanaunga mkono juhudi za Rais John Magufuli.
UPDATE
Mgombea wa Udiwani Hamid Mfalingungi amepatikana akiwa kituo cha polisi, hajaruhiswa kuzungumza na mtu yoyote.
Amebainisha kwamba kwa sasa wanawasiliana na makao makuu ya chama ili waweze kupata msaada wa kisheria wa kujua jambo gani la kufanya kuweza kupata haki yao.
Giza latanda CHADEMA, mgombea atoweka
Reviewed by KUSAGANEWS
on
July 14, 2018
Rating:
No comments:
Post a Comment