Katibu Mkuu wa Chadema Dk Vincent Mashinji na
viongozi wengine wa chama hicho jana walikaa kwa zaidi ya saa moja katika ofisi
za Tume ya Taifa ya Uchaguzi(Nec), wakilalamikia hujuma katika uchaguzi mdogo
wa Agosti 12
Dk Mashinji na viongozi hao walipeleka ushahidi wa barua za
malalamiko ya hujuma wanazodai kufanyiwa katika uchaguzi huo
Uchaguzi unaofanyika Agosti 12, 2018, ni wa jimbo la
Buyungu, Kigoma na kata 77 baada ya madiwani wengi, kuhama vyama vya upinzani
na kuhamia CCM wakidai wanaunga mkono juhudi za Rais John Magufuli
Aliyekuwa Mbunge wa Buyungu, Kigoma, Kasuku Bilago amefariki
dunia Mei mwaka huu
Dk Mashinji alisema walifika katika ofisi hizo leo Julai 14
saa 4:50 asubuhi na waliamua kuondoka saa 6:45 mchana baada ya
kuelezwa kwamba Mkurugenzi wa Uchaguzi, Dk. Athumani Kihamia asingeweza kuonana
nao
“Tulikuwa na barua mbili mkononi kama ushahidi wa nakala za
madai tulizotuma kwa mkurugenzi huyo siku tatu zilizopita kuhusu hujuma katika
kata tano za halmashauri ya Tunduma,” alisema
Alizitaja kata hizo ni ya Kaloleni, Majengo, Sogea, Mpemba
na Mwaka wa Kati.
“Tulifika pale tukiwa na barua zetu mbili, tulitaka
kumuonyesha ushahidi wa nakala ya barua hizi ambazo anasema hazitambui,
tumefika pale msaidizi wake akatusikiliza na kuchukua taarifa zetu, akampelekea
akiwa katika kikao cha menejimenti, tumesubiri baadaye saa moja
imepita(Mkurugenzi) anatuma ujumbe kwamba hawezi kuonana na sisi,”alisema Dk
Mashinji.
Chadema washinda ofisi za NEC wakilalamikia rafu uchaguzi wa Agosi 12
Reviewed by KUSAGANEWS
on
July 14, 2018
Rating:
No comments:
Post a Comment