Baraza la wafugaji katika mamlaka ya hifadhi ngorongoro
limefanya mkutano kwa ajili ya kufanya marekebisho katiba inayoendana na
kipindi cha sasa baada ya kutumia katiba
ya muda mrefu ambayo haikuwa imeshirikisha maoni ya wanachi.
Akizungumza Mwenyekiti wa baraza la wafugaji Wilayani
Ngorongoro Bwana Edward Maura amesema lengo la kubadili katiba ni kwasababu
tangu mamlaka hiyo ianzishwe mwaka 2000 mamlaka haijawahi kufanya marekebisho
yeyote.
Maura amesema katiba ya zamani ina mapungufu kwasababu
ilikuwa inataja idadi ya vijiji ambavyo
vinatakiwa kushiriki kwenye baraza lakini kwa mujibu wa sheria za mitaa vijiji
vimekuwa vikiongezeka hivyo kuna baadhi ya vijiji vilivyopo ambavyo viko ndani
ya mamlaka na havishiriki katika mbaraza.
Amesema wanatafuta katiba ambayo inaendana na serikali
ya awamu ya tano na itakayokidhi mahitaji ya watu bila kuathiri uwepo wa baraza
na kupunguza garama za uendeshaji ili fedha ziende kwa walengwa maskini ambao
ndiyo wanaolengwa na serikali.
Maura amesema katiba ambayo walikuwa wanaitumia tangu
mwaka 2000 ilikuwa haijashirikisha maoni ya wananchi lakini ambayo kwasasa
wanaifanyia marekebisho itakuwa imefanya inamgusa moja kwa moja wananchi.
Akitoa maoni yake mjumbe wa baraza la Wafugaji ambaye
pia ni mbunge wa Ngorongoro Mh William Olenasha amesema kuwa kupitia mabadiliko
hayo ya katiba itakuwa na msaada mkubwa kwasababu imeshirikisha wananchi ambao
ndiyo walengwa.
Olenasha amesema kuwa baraza la wafugaji linatakiwa kuwa
chachu ya kusaidia maendeleo kwa jamii na kulinda vyanzo vikuu vya kiuchumi kwa
wenyeji kama ufugaji wa asili ikiwemo mila na Desturi zilizopo.
Baadhi ya wajumbe wakichangia katika mkutano huo
wamesema kuwa kuwepo kwa mabadiliko ya katiba itakuwa ndiyo kiunganishi kikubwa
kati ya wananchi ambao ndiyo wanatakiwa kunufaiki na mamlaka kwasababu wako
ndani ya mamlaka ya Hifadhi.
Wamesema kuwa kupitia katiba hiyo kutasaidia kuangalia
walipo toka na wanapokwenda kwa kulinda misingi iliyoainishwa kisheria na
mamlaka ya hifadhi bila kuathiri wananchi wa hali ya chini.
Baraza la Wafugaji Ngorongoro lafanya marekebisho ya Katiba
Reviewed by KUSAGANEWS
on
July 14, 2018
Rating:
No comments:
Post a Comment