Wasichana zaidi ya
17,840, Mkoani Iringa wanatarajiwa kupata chanjo ya Saratani ya Mlango wa Uzazi
ifikapo mwishoni mwa mwezi April mwaka huu.
Mratibu wa Afya Mkoani humo, Naftali
Mwalongo, amebainisha hayo wakati wa kikao cha uzinduzi wa kamati ya
uhamasishaji Mkoani Iringa kuwa chanjo ya HPV itatolewa kwa awamu ikiwa na
lengo la kutoa kinga kwa watoto wa kike wenye umri kati ya miaka 9 hadi14.
Kwa upande wake, Kaimu Katibu Tawala
Mkoa wa Iringa, Lukas Kambelenje, amesema ni mara ya Kwanza chanjo ya HPV
kufanyika Mkoani humo,
Aidha ameitaka Kamati hiyo
kutoa ushirikiano wa kutosha katika kuhamasisha wazazi kuwapeleka watoto wao
kupata Chanjo hiyo
Wasichana 17,840 Iringa kupata neema
Reviewed by KUSAGANEWS
on
March 22, 2018
Rating:
No comments:
Post a Comment