Uchumi wa Ujerumani
unazidi kuimarika lakini takwimu mpya zilizotolewa na ofisi ya kazi ya
shirikisho iliyogusiwa bungeni na chama cha mrengo wa kushoto Die Linke
zinaonesha kwamba kuna watu 153,950 ambao bado wanaishi bila ajira kwa kipindi
cha alau miaka mitano.
Mbunge wa chama hicho
Sabine Zimmermman ameitaja hali hiyo nchini Ujerumani kuwa ni kashfa
kubwa.Mnamo mwezi Januari idadi ya watu waliokuwa hawana ajira kwa zaidi ya
mwaka mmoja ilikuwa zaidi ya watu 868,000.
Kwa mujibu wa kiongoni
wa vyama vya CDU/CSU bungeni Volker Kauder, serikali mpya ya muungano nchini
Ujerumani kati ya vyama vya Social Democratic SPD na vyama ndugu vya Christian
Democratic Union CDU na Christian Social Union CSU inataka kuweka mbele masuala
ya muda mrefu ya ukosefu wa ajira akisema kwamba ukosefu wa ajira ni changamoto
kubwa.
Ukosefu wa ajira Ujerumani ni kashfa kwa serikali
Reviewed by KUSAGANEWS
on
March 08, 2018
Rating:
No comments:
Post a Comment