Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa
na Michezo Dkt. Harrison Mwakyembe ameeleza kupokea kwa masikitiko kifo cha
mchezaji wa Tanzania wa mpira wa kikapu Bi Yvvone Christopher Wambura.
Yvonne alifariki dunia Machi 21
jijini Dar es salaam ambapo kabla ya kifo alikuwa mchezaji wa timu ya JKT
Queens ambayo ilikuwa inashiriki ligi ya kikapu mkoa wa Dar es salaam.
Mwakyembe amesema taifa limepoteza
mtu muhimu aliyekuwa anajitoa kwaajili ya timu yake ya taifa kwa ujumla huku
akitoa pole kwa familia pamoja na Jeshi la Kujenga Taifa.
Mwakyembe aguswa kifo cha mchezaji
Reviewed by KUSAGANEWS
on
March 23, 2018
Rating:
No comments:
Post a Comment