Makamu wa Rais wa Tanzania na Samia
Suluhu Hassan amewata wanachama wa CCM Kisiwani Pemba kuwa kitu kimoja kuelekea
Uchaguzi Mkuu wa 2020 ili waweze kunyakua majimbo mengi.
Mh. Samia ametoa kauli hiyo
alipokuwa akizungumza na wanachama wa chama hicho Jimbo la Ole, Wilaya ya
Chakechake baada ya kuweka jiwe la msingi la tawi la CCM, amesema kitendo cha
wanachama wa chama hicho kutokuwa na furaha katika kisiwa hicho ni miongoni mwa
sababu zinazowafanya washindwe kujipanga na hatimaye chama cha upinzani
kushinda katika majimbo yote.
Amesema anajua ndani ya CCM wapo
baadhi ya watu hawana hamasa, jambo ambalo linaonyesha ni kama chama hicho
hakipo kwenye jimbo hilo na maeneo mengine ya Pemba na kusahau kuwa CCM ndicho
chama pekee kinachoongoza Serikali.
Mama Samia amebainisha kuwa, kuna
baadhi ya wanachama wamekuwa wakila kiapo cha kukilinda chama, lakini kinyume
chake hushindwa kutekeleza majukumu yao kutokana na kile alichokiita kuwa ni
woga usiokuwa na tija. “Ni lazima vijana wa CCM mjenge ujasiri na
uthubutu"
Pamoja na hayo, amewataka wana CCM
kisiwani humo kuacha tabia ya kuwatenga wanachama wa vyama vya upinzani, badala
yake wawashawishi ili wajiunge kwenye chama chao alichokitaja kuwa ni bora
zaidi na chenye kujali masilahi ya wananchi wote.
Mama Samia Asemea udhaifu wa CCM
Reviewed by KUSAGANEWS
on
March 23, 2018
Rating:
No comments:
Post a Comment