Jeshi la Polisi mkoani Singida
limetoa taarifa juu ya ajali ya moto ambayo iemeteketeza lori mapema hii leo,
na kusababisha vifo vya watu walikuwamo kwenye lori hilo.
Akizungumza
Kamanda wa Polisi mkoa wa Singida Debora Magiligimba, amesema ajali hiyo
imetokea leo majira ya saa nne asubuhi, baada ya lori hilo kuacha njia na
kupinduika na kisha kuwaka moto, na kusababisha vifo vyta dereva na konda wake
ambao wote ni wakazi wa Dar es salaam.
“ Lori lenye namba T 167 DQT aina ya
flight liner mali ya Petrolmark Afrika ya jijini Dar es salaam, liliacha njia
na kupinduka na kisha kuungua, watu waili ambao ni wanaume waliokuwamo
wamefariki, uchunguzi wa jeshi la polisi baada ya kupita mzani wa Singida saa 1
asubuhi, gari hiyo ilikuwa inaendeshwa na Erasto Abedi Rusazi na Ramadhani
Hashim Ramadhani wote wakazi wa Dar es salaam, na lilikuwa limebeba mafuta”,
amesema Kamanda Magiligimba.
Kamanda Magiligimba amesema miili ya
marehemu imehifadhiwa katika hospitali ya willaya ya Kiomboi, na ndugu zao
wanaombwa kwenda kutambua miili.
Jeshi la polisi latoa ripoti ya lori linaloungua
Reviewed by KUSAGANEWS
on
March 23, 2018
Rating:
No comments:
Post a Comment