Mahakama moja mjini Baghdad imemuhukumu adhabu ya kifo kwa tuhuma za ugaidi nduguye wa kike aliyekuwa kiongozi wa kundi la mtandao wa kigaidi la Alqaeda nchini Iraq aliyeuwawa mwaka 2010.
Msemaji
wa baraza kuu la sheria nchini Iraq Abdul- Sattar Bayrkadar amesema kupitia
taarifa kwamba dadake Abu Omar al Baghdad amekutwa na hatia kwa kuhusika kutoa
msaada wa usafiri pamoja na msaada wa aina yningine wanamgambo katika
kufanikisha vitendo vya uhalifu.
Mwanamke
huyo ambaye jina lake halikutajwa pia alikutwa na hatia ya kugawa fedha
miongoni mwa wanamgambo mjini Mosul. Hata hivyo hakufafanuliwa kuhusu mashtaka
hayo na muda bibi huyo aliowahi kushirikiana na kundi la al Qaida nchini Iraq.
Hata
hivyo Baykdar amesema kwamba mumewe mwanamke huyo alihukumiwa kifo akiwa kama
mwanachama wa uongozi wa kundi hilo la kigaidi. Albaghdad aliuwawa Aprili 2010.
Dadake Al Baghdad ahukumiwa kifo Iraq
Reviewed by KUSAGANEWS
on
March 08, 2018
Rating:
No comments:
Post a Comment