Mamlaka ya Kodi ya mapato(TRA) mkoa
wa Arusha, imewataka wafanyabiashiara ,wakiwepo wamiliki wa Bar na nyumba za
kulala wageni, kutumia mashine ya kielekroniki kwa kutoa risiti kwa wateja ili
kuepuka kupigwa faini kati ya sh 3 milioni hadi 4.5 milioni kwa
watakaomatwa hawatumii mashine .
TRA mkoani hapa imeanza msako
mchana na usiku katika maeneo yote ya mkoa wa Arusha ili kuwakatama
wafanyabiashara ambao wamekaidi kutumia mashine za EFD.
Meneja wa TRA mkoa wa Arusha,Apili
Mbaruku alitoa wito huo wakati anazungumza na Jumuiya ya wafanyabiashara mkoani
Arusha,katika semina maalum ya kuwaelimisha juu ya matumizi ya mashine hizo za
EFD.
Mbaruku alisema, kila bidhaa
inayouzwa inapaswa kutolewa risiti, zikiwepo Bia hivyo, maafisa wa TRA
watafanyakazi usiku na mchana kuhakikisha wafanyabiashara wote ambao
wanahitajika kutumia mashine hizo wanatumia.
"hatupendi kuwapiga faini
lakini italazimika kufanya hivyo, kwani tunasimamia sheria na imeonekana idadi
kubwa yawafanyabiashara mkoani hapa hawatumii mashine za EFD kama ambavyo
inatakiwa"alisema
Awali, Msimamizi mkuu wa mradi wa
matumizi ya EFD mkoani Arusha, Alphael Mollel alisema, maafisa wa TRA mkoani
Arusha, wameanza msako kwa ambao hawatumii mashine na wasilaumiwe kwa kazi
hiyo.
"tayari tumeanza kukamata watu,
wanakuja ofisini wanalia lakini, tunawaambia hakuna jinsi lazima walipe faini
milioni 3 ama milioni 4.5 hindwa tutachukuwa hatua ikiwepo kufunga biashara
"alisema
Meneja Huduma kwa
Wateja wa TRA Arusha, Regina Mkumbo alisema, mkoa wa Arusha kuna mawakala zaidi ya 10 ambao
wanauza mashine za EFD hivyo, hakuna sababu ya afanyabiashara kushindwa kununua
kwa wakati.
Hata hivyo, alisema
kwa ambao mashine zao zimeharibika wanapaswa kutoa taarifa TRA kwa barua na
sehemu waliyonunua mashine ili kuhakikisha hawapigwi faini kwa kutotumia
mashine.
Mwenyekiti wa
wafanyabiashara mkoa wa Arusha, Locken Adolf aliwawaka wafanyabiashara kufuata
sheria ili kuondoa migogoro na serikali, kwani tayari sheria ya matumizi ya
lazima ya EFD imepitishwa.
"ni ukweli jambo
hili limekaa pabaya lakini hatuna jinsi lazima tutumie mashine kwani pia
zinasaidia kutunguza makadilio makubwa ya kodi ambao tumekuwa
tukifanyiwa"alisema.
TRA Arusha yawaonywa wafanyabiashara kwa kutotumia mashine za EFD
Reviewed by KUSAGANEWS
on
July 09, 2017
Rating:

No comments:
Post a Comment