Mtangazaji wa EFM, maarufu Bikira wa Kisukuma, afariki dunia Muhimbili


Taarifa za kifo chake zimethibitishwa leo Jumapili, Julai 9, na  redio ya EFM kupitia ukurasa wake wa  Instagram.Mmoja wa watangazaji wa habari za michezo ya Efm, Maulid Kitenge ameandika katika ukurasa wake wa Twitter, akisema; Sad news…Seth Bikira wa Kisukuma hatunaye.

Aliyekuwa mtangazaji wa radio ya EFM, Sethi Katende, (maarufu kama Bikira wa Kisukuma) amefariki dunia leo katika Hospitali ya Taifa ya Muhimbili.

Taarifa za kifo chake zimethibitishwa leo Jumapili, Julai 9, na  redio ya EFM kupitia ukurasa wake wa  Instagram.

Mmoja wa watangazaji wa habari za michezo ya Efm, Maulid Kitenge ameandika katika ukurasa wake wa Twitter, akisema; Sad news…Seth Bikira wa Kisukuma hatunaye.”

 Marehemu alikuwa akitangaza kipindi cha ‘Ubaoni’kinachorushwa na Redio hiyo  akiwa na wenzake watatu, Mpoki au Mwarabu wa Dubai na Imma Kapanga.

Taarifa zilizotolewa na redio hiyo, zimeeleza kuwa mwili wa marehemu umepelekwa nyumbani kwa baba yake mzazi, Changanyikeni kwa ajili ya taratibu za mazishi.

 

 


Mtangazaji wa EFM, maarufu Bikira wa Kisukuma, afariki dunia Muhimbili Mtangazaji wa EFM, maarufu Bikira wa Kisukuma, afariki dunia Muhimbili Reviewed by KUSAGANEWS on July 09, 2017 Rating: 5

No comments: