WAFANYABIASHARA wa mahoteli na
nyumba za kulala wageni manispaa ya Morogoro juzi pasipo taarifa yoyote
wamejikuta wakipoteza mapato yao yanayokadiriwa kufikia shilingi mil.200 baada
ya halimashauri hiyo kudaiwa kujichukulia sheria mkononi na kuzifunga kwa
makufuri hoteli na gesti zaidi ya 20.
Baadhi yao wakiungwa mkono na
viongozi wao akiwemo Katibu wa chama-MOGOA, Mtei Mtei walisema zoezi hilo
lililofedhesha kazi zao hizo lilianza 6.Julai asubuhi kwa maofisa
waliojitambulisha kutoka Manispaa hiyo kufika sehemu zao za biashara na
kuzifunga makufuli milango yote kwa madai hawajalipa tozo ya hoteli ‘Hotel
levy’.
“Tumeshangazwa na tozo hii,kwanza
ilishafutwa na Tamisemi tangu mwaka 2013na halmashauri kuagizwa kukaa na sisi
ili kuona namna ambavyo tutaiwezesha halamashauri kupata fedha na tulisha
kubaliana asilimia 10 ya pato kwa mwaka badla ya 20 ya awali” alifafanua
wafanya biashara mmoja.
Kwa upande wake katibu wa Mogoa,
Mtei alisema kimsingi wakotayari kulipa tozo waliyokubaliana kuiongezea
halmashuri pato kwa mwaka ila yenyewe imekuwa haitaki maelewano na wao jambo
ambalo limewasababishia kufikishana mahakamani dhiidi ya mambo hayo.
Katika ufafanuzi wake katibu huyo
alisema wafanya biashara hao wamefedheheka baada ya baadhi ya hoteli kufungiwa
milango huku zikiwa na wageni,huku hoteli na nyumba nyingine za kulala wageni
zikishindwa kuendeleza maombi zilizokuwa zimepata kutoka kwa wateja wao wanao
waamini.
“unajua kipindi hiki ni cha mzunguko
mkubwa wa fedha wazazi wanapeleka watoto mashuleni hivyo wanalazimika kulala
mjini,kuna watalii na Mikumi,Udizungwa na Serous wamekosa huduma,kuna bokingi
za kumbi kwa sherehe na mikutano ambapo pia walipaswa kulisha washriki,hayo
yote na mengineo fedha tumepoteza”alifafanua Mtei.
Hata hivyo alisema kwa sasa chama
kimewashuri waathirika mmoja mmoja kumfungulia mashitaka Mkurugenzi wa Manspaa
hiyo sambamba na kuitaka mahakama kutafsiri sheria juu ya nani mwenye mamlaka
ya kufunga shuguli ya mtu kisheria.
Alipotafutwa mkurugenzi wa manspaa
hiyo John Mgalula hakupatikana ofisini kwake na hata alipotafutwa kwa simu yake
ya kiganjani pia haikuwa na majibu yoyote,hata hivyo Meya Paschal Kihanga
alikana kuwepo kwa zoezi bila taarifa akisisitiza kuwa hilo ni agizo la kamati
ya fedha mwishoni mwa wezi uliopita likiwataka watendaji kukusanya madeni yote.
“sikwepo kwa muda mrefu na nikili
kuwa zoezi hili binafsi silifahamu vema na sikweli kuwa linafanyika bila
taarifa isipokuwa ninachokumbuka ni kuwa mwishoni mwa mwezi uliopita kwenye
kamati ya fedha tulimwagiza mkurugenzi kukusanya haraka madeni yote ya fedha
zilizo nje…inawezekana huo ndio utekelzaji wake”alifafanua Kuhanga.
MANISPAA MOROGORO WAFUNGIA NDANI WATEJA MAHOTELINI WAKIDAI 'HOTEL LEVY
Reviewed by KUSAGANEWS
on
July 09, 2017
Rating:

No comments:
Post a Comment