Wanahabari wa runinga ya Reuters, wamepata maiti ya wanaume, wanawake na watoto, zikiwa zimetapakaa katika barabara za mji huo.
Hilo limetokea katika Wilaya ya Zanjili, karibu na eneo la mapigano, ambapo jeshi la taifa ya Iraq, linakabiliana vikali na wanamgambo hao wa Dayesh, kama wanavyofahamika.
Mfanyakazi mmoja wa shirika la utoaji misaada la Marekani- Dave Eubank, amesema kuwa wapiganaji wa I-S, wamekuwa wakiwamiminia risasi wananchi wanaojaribu kuutoroka mji huo.
Amesema kuwa ameona maiti 50, lakini kwa msaada wa jeshi la Marekani linalosaidiana na wanajeshi wa Iraq, amefaulu kuwaokoa watu wawili tu.
Raia 50 wameuwawa Mosul, Iraq
Reviewed by KUSAGANEWS
on
June 04, 2017
Rating:
No comments:
Post a Comment