Mbunge wa Kibamba, John Mnyika ametolewa nje ya Bunge leo
Ijumaa kwa agizo la Spika wa Bunge, Job Ndugai.
Licha ya adhabu hiyo, amemzuia kutohudhuria vikao vya Bunge
kwa siku saba kuanzia leo.
Mnyika ametolewa baada ya mmoja wa wabunge kusema 'Mnyika
mwizi' akimhusisha na wizi wa madini, hoja inayochangiwa na wengi kwenye mjadala
wa Wizara ya Nishati na Madini unaoendelea.
Kutokana na hali hiyo Mnyika alimtaka Spika kuchukua hatua
kwa mbunge aliyesema kuwa yeye ni mwizi lakini Spika akasema hajui hilo na
haijaingia kwenye hansadi. Hata hivyo Mnyika alisisitiza kuwa mambo hayaweze
kwenda hivyo.
Baada ya majibizano kati yake na Spika, Spika akaamuru
walinzi wamtoe Mnyika nje ya Bunge na asihudhurie vikao saba vinavyofuata.
Mnyika alikuwa akitoa maelezo baada ya Mbunge wa Mtera,
Livingston Lusinde kusema upinzani wa Tanzania ni wa ajabu kwani unatetea wezi
wa madini.
MBUNGE WA KIBAMBA (CHADEMA) JOHN MNYIKA AONDOLEWA BUNGENI
Reviewed by KUSAGANEWS
on
June 02, 2017
Rating:

No comments:
Post a Comment