MAZISHI ya Mbunge mstaafu wa jmbo la Moshi mjini na
Mwenyekiti wa Chadema mkoa wa Kilimanjaro Philemon Ndesamburo Kiwelu (82)
yanatarajiwa kufanyika kwa siku mbili mfululilizo huku watu zaidi ya laki 2
wakitarajiwa kushiriki katika mazishi hayo.
Shughuli nzima za mazisihi zinataraji kufanyika June 5 na
sita katika uwanja wa mashujaa mjini Moshi kabla ya kuhitimishwa siku ya
Jumanne kwa ibada itakayoanzia kanisani na kumalizikia nyumbani kwa
marehemu.
Hatua ya maziko ya Ndesamburo kufanyika kwa siku mbili
inatokana na uwepo wa idadi kubwa ya marafiki wa familia kushiriki katika
maziko hayo ya kihistoria yatakayotanguliwa na kutoa heshima za mwisho
,shughuli zilizopangwa kufanyika katika uwanja wa mashujaa mjini Moshi.
Akizungumza mara baada ya kumalizika kwa kikao kilichodumu
kwa zaidi ya saa nne ,Msemaji wa Chadema katika maandalizi ya mazishi hayo
Amani Golugwa amesema uamuzi huo unatokana na kutoa nafasi kwa watu mbalimbali
kutoa heshima za mwisho kwa Ndesamburo.
“Tumekua na kikao na wanafamilia viongozi wa chama na
mashaurizano kuhusiana na msiba huu ,tumekuwa na watoto wa marehemu ,walikuwepo
wachungaji na viongozi wa chama ,kimsini tumekubaliana mazishi ya mze wetu
Ndesamburo yatafanyika kwa siku mbili mfululizo”alisema Golugwa.
Kutakuwa na siku mbili za maombolezi,siku ya jumatatu mwezi
huu tutakuwa na state funeral (mazishi ya kitaifa) siku ambayo tutafanya
kumbukizi ya maisha yake na tunataraji kuwa na idadi kubwa sana ya watu”alisema
Golugwa.
Kwa upande wake msemaji wa familia ambaye pia ni motto
mkubwa wa marehemu Ndesamburo,Sindato Ndesambur o alisema vikao mbalimbali
vinaendelea kwa ajili ya maandalzi ya mazishi na kwamba yanataraji kutanguliwa
na maandamano.
“Kama unavyoona bado tunaendelea na vikao kwa sasa ,kuona
namna gani tunaweza kumuaga mzee wetu kwa heshima aliyojijengea kwa wakazi wa
Moshi na taifa kwa ujumla “alisema Sindato.
Alisema wanatazamia kupokea wageni wengi kutoka ndani na nje
ya nchi zikiwemo taasisi mbalimbali za kidini,kiserikali pamoja na
wafanyabiashara watakao shiriki katika shughuli nzima ya mazishi .
Mapema jana vilio na Simanzi vilitawala chumba cha
kuhifadhia maiti katika Hospitali ya Rufaa ya KCMC ,wakati familia ya Marehemu
Ndesamburo ikiongozwa na mtoto wake wa Pili ,Lucy Owenya kushudia mwili wa
mpendwa wao ukiwa umehifadhiwa.
Wakati kifo cha Mzee Ndesamburo kinatokea ,Lucy Owenya
alikuwa akihudhuria vikao vya Bunge la 11 ,vikao vya Bajeti ambapo alipata
nafasi ya kuchangia mjadala wa bajeti ya wizara ya fedha kabla ya kupokea
taarifa rasmi ya kifo cha Ndesamburo ambaye pia ni mfanyabiashara mashuhuri.
Majira ya saa 11:45 familia ilifika katika hospitali ya
rufaa ya KCMC huku Mbunge wa jimbo la Rombo ,Joseph Selasini akisimamia zoezi
la kuomba kuona mwili wa marehemu Mzee Ndesamburo ili kujiridhisha kama kweli
baba yao amelala mauti.
Philemoni Ndesamburo atakumbukwa na mengi hasa katika siasa
za mageuzi ambapo katika uchaguzi wa mwaka 2015 akiwa ni mwenyekiti wa Chadema
mkoa wa Kilimanjaro alisaidia kupatikana kwa madiwani wengi katika baraza la
madiwani wa manispaa ya Moshi.
Ndesamburo maarufu kama Ndesa Pesa ametumia muda wake mwingi
katka siasa na biashara ,amefariki dunia wakati akitaka kukabidhi mchango wake
kwa meya wa jiji la ARUSHA ,Kalist Lazaro kwa ajili ya familia za watoto wa
shule ya msingi ya Lacky Vicent waliofariki katika ajali ya gari Wilayani
Karatu mkoani Arusha.
MAZISHI YA KIGOGO WA CHADEMA KUFANYIKA SIKU MBILI MFULULIZO
Reviewed by KUSAGANEWS
on
June 02, 2017
Rating:

No comments:
Post a Comment