JESHI la Polisi nchini limekemea tabia inayoendelea kujengeka miongoni mwa baadhi ya wananchi ya kutoheshimu sheria na kujichukulia sheria mikononi kwa kuwapiga, kuwadhalilisha watuhumiwa, kuwachoma na kuwaua.
Aidha imetangaza zawadi kwa mwananchi yeyote atakayerekodi tukio la aina hiyo na kulifikisha kwao.
Imeelezwa kuwa kuanzia Januari hadi Oktoba mwaka huu, watuhumiwa 829 wameuawa na wananchi.
Imeelezwa kuwa kuanzia Januari hadi Oktoba mwaka huu, watuhumiwa 829 wameuawa na wananchi.
Polisi
imewaomba wananchi kutoa ushirikiano wa kutosha kukomesha tabia hiyo na
kuahidi kuwa mwananchi yeyote atakayerekodi tukio la watu
wanaojichukulia sheria mkononi na kulifikisha polisi kwa siri atapewa
zawadi.
Akizungumza
na waandishi wa habari jana Dar es Salaam, Msemaji wa jeshi hilo,
Advera Bulimba alisema idadi ya watu hao waliokufa imeongezeka
ikilinganishwa na watuhumiwa 785 waliouawa kwa sababu kama hizo kwa
kipindi kama hicho mwaka 2014.
“Katika
siku za hivi karibuni, kumeibuka tabia hiyo ya wananchi kujichukulia
sheria mkononi na kuwafanyia vitendo vya kikatili ikiwemo kuwadhalilisha
kwa kuwavua nguo watuhumiwa wanaoshukiwa kujihusisha na vitendo vya
kihalifu bila kuwafikisha kwenye vyombo vya dola jambo ambalo ni kinyume
cha sheria, kanuni na taratibu za nchi,” alifafanua msemaji wa Polisi.
Alisema
takwimu zinaonesha wazi kwamba tabia hiyo inaendelea kujengeka na
kuonekana kwamba ni jambo la kawaida, lakini ni ukiukwaji mkubwa wa
taratibu na sheria za nchi.
Bulimba
alisema makamanda wote wa polisi nchini wameagizwa kufanya ukamataji wa
watu wote wanaojihusisha na vitendo vya kihalifu kwa kisingizio cha
hasira kali na kuwafikisha mahakamani kwa sababu watu hao kwa mujibu wa
sheria, tayari wanakuwa wametenda kosa la jinai.
'Ukimrekodi Mtu Anayejichukulia Sheria Mkononi Utapewa Zawadi Nono na Jeshi la Polisi'
Reviewed by KUSAGANEWS
on
November 24, 2015
Rating:
No comments:
Post a Comment