Rais Magufuli Afuta sherehe za Maadhimisho ya siku ya UKIMWI Kitaifa......Aagiza Fedha za Maandalizi ya Sherehe Hizo Zikanunulie Dawa za Waathirika
Rais
John Magufuli amesitisha maadhimisho ya siku ya Ukimwi kitaifa ambayo
yalikuwa yafunguliwe mkoani Singida jana na kufikia kilele chake Desemba
mosi mwaka huu mjini humo.
Badala
yake Rais Dk Magufuli ameagiza fedha zote ambazo zilitengwa na serikali
pamoja na wahisani mbalimbali kwaajili ya maadhimisho hayo zielekezwe kununua dawa kwaajili ya waathirika wa Ukimwi na vitendanishi.
Akizungumza
na moja kwa moja na Televisheni ya Taifa (TBC), Mwenyekiti Mtendaji wa
Tume ya Taifa ya Kudhibiti Ukimwi (TACAIDS), Dk Fatma Mrisho, amesema
serikali imetoa agizo hilo jana wakati tayari mkuu wa Mkoa wa Singida
akiwa ameshafungua maonesho ya maadhimisho hayo.
“Serikali
imesitisha maadhimisho ya mwaka huu Singida na badala yake fedha
zilizopangwa kwaajili ya maadhimisho ziende zikanunue dawa za virusi vya
Ukimwi, dawa za kudhibiti maambukizi ya ukimwi na vitenganishi,” amesema Mrisho.
Dk
Mrisho amesema kuwa tayari taarifa za kusitisha maadhimisho hayo
zimesha wafikia washiriki na wale walio kuwa njiani kuelekea Singida
wamegeuza.
Akizungumza
na waandishi wa habari ofisini kwake Dar es Salaam juzi kabla ya
sherehe hizo kusitishwa, Mwenyekiti Mtendaji wa Tume ya Taifa ya
Kudhibiti Ukimwi (TACAIDS), Dk Fatma Mrisho alisema maadhimisho ya mwaka
huu yalikuwa yatanguliwe na maonesho ya wadau yatakayojumuisha huduma
mbalimbali zikiwamo za utoaji elimu na burudani.
Dk
Mrisho alisema huduma nyingine zilizopangwa kutolewa katika maadhimisho
hayo ya wiki moja ni upimaji wa hiari wa watu zaidi ya 3,500 wanaoishi
na virusi vya Ukimwi na utoaji ushauri nasaha, upimaji wa shingo ya
uzazi, sukari, uzito, damu na kupata elimu itakayotolewa kupitia vikundi
vya sanaa na burudani.
Maadhimisho
ya mwaka huu yanachagizwa na kaulimbiu ya ‘Tanzania bila maambukizi
mapya ya VVU, vifo vitokanavyo na Ukimwi na ubaguzi na unyanyapaa
inazewekana.’
Mkuu
wa Mkoa wa Singida, Dk Parseko Kone aliwaambia waandishi wa habari
ofisini kwake hivi karibuni kuwa maadhimisho hayo yanatarajiwa kuanza
Novemba 24 mwaka huu kwenye viwanja vya Peoples Club ambapo uzinduzi
utakuwa Novemba 25 kabla ya kilele, Desemba mosi.
Hii
ni mara ya tatu tangu Rais Dk Magufuli aingie madarakani kuzuia
maadhimisho yanayogharimu fedha nyingi za sherehe na fedha zake
kuelekeza ikanunulie vifaa tiba mahospitalini.
Awali
Rais aliagiza fedha zilizotengwa kwaajili ya hafla ya uzinduzi wa Bunge
zaidi ya shilingi Milioni 225 ziende kununulia vitanda vya hospitali ya
taifa Muhimbili.
Aidha
Rais pia alisitisha maadhimisho ya siku ya Uhuru Desemba tisa mwaka huu
na badala yake watu wafanye kazi katika maeneo yao ya kazi hasa usafi
wa mazingira.
mpekuzi
Rais Magufuli Afuta sherehe za Maadhimisho ya siku ya UKIMWI Kitaifa......Aagiza Fedha za Maandalizi ya Sherehe Hizo Zikanunulie Dawa za Waathirika
Reviewed by KUSAGANEWS
on
November 26, 2015
Rating:
No comments:
Post a Comment