Kesi
ya kupinga matokeo ya uchaguzi iliyofunguliwa na aliyekuwa Mbunge wa
Kigoma Kusini (NCCR-Mageuzi), David Kafulila, kupinga matokeo ya
uchaguzi itaanza kusikilizwa leo na Jaji John Utamwa katika Mahakama Kuu
ya Tanzania, Kanda ya Tabora.
Kafulila
aliyekuwa Mbunge kinara katika kuibua ufisadi wa sakata la uchotwaji wa
zaidi ya Sh. bilioni 306 katika akaunti ya Tegeta Escrow iliyokuwa
Benki Kuu ya Tanzania (BoT), anakutana ‘uso kwa uso’ na Jaji Utamwa,
ambaye ndio alitoa hukumu tata iliyosababisha kuibuka kwa kashfa ya
ufisadi wa fedha hizo.
Jaji
Utamwa aliitoa hukumu hiyo, Septemba 8, 2013 kwa kumwamuru Kabidhi
Wasihi, kukabidhi mtambo wa Kampuni ya kufua umeme wa dharura ya
Independent Power Tanzania Limited (IPTL) kwa mmiliki wake mpya ambaye
ni kampuni ya Pan Africa Power Solutions Tanzania Limited (PAP) baada ya
kukubaliana na maombi ya aliyekuwa mbia wa IPTL, kampuni ya Engineering
and Marketing Limited (VIP) iliyoondoa kesi yake kwa lengo la kuifilisi
IPTL.
Hukumu
hiyo ndio ilikuwa chanzo cha Kafulila kuibua kashfa hiyo bungeni kwa
kuwahusisha vigogo mbalimbali wa serikali na ufisadi huo.
Mpekuzi blog
Jaji wa Escrow Kusikiliza Kesi ya Ubunge wa David Kafulila
Reviewed by KUSAGANEWS
on
November 26, 2015
Rating:
No comments:
Post a Comment