Hapa Kazi Tu: Serikali Yapiga Marufuku Utengenezaji na Uchapishaji Kadi za Xmass na Mwaka Mpya kwa Gharama Zake
Katibu
Mkuu Kiongozi Balozi Ombeni Sefue amepiga marufuku utengenezaji na
uchapishaji wa kadi za Christmas na Mwaka Mpya kwa gharama za
serikali/umma, kwa mwaka huu.
Balozi Sefue, ameelekeza kuwa yeyote anayetaka kutengeneza ama kuchapisha kadi hizo, afanye hivyo kwa gharama zake mwenyewe.
Badala
yake Balozi Sefue ameagiza fedha zilizopangwa kugharamia utengenezaji
na uchapishaji wa kadi, zitumike kupunguza madeni ambayo Wizara, Idara
na Taasisi za umma zinadaiwa na wananch/wazabuni waliotoa huduma na
bidhaa kwao au zipelekwe katika matumizi mengine ya kipaumbele.
Gerson Msigwa
Kaimu Mkurugenzi wa Mawasiliano, IKULU
26 Novemba, 2015
Kaimu Mkurugenzi wa Mawasiliano, IKULU
26 Novemba, 2015
Mpekuzi blog
Hapa Kazi Tu: Serikali Yapiga Marufuku Utengenezaji na Uchapishaji Kadi za Xmass na Mwaka Mpya kwa Gharama Zake
Reviewed by KUSAGANEWS
on
November 26, 2015
Rating:
No comments:
Post a Comment