CHADEMA YASHINDA KESI YA KUAGA MWILI WA MAWAZO...HUKUMU YAFAFANUA."Kazi ya Polisi ni kulinda raia na si kuzuia mazishi.."
Taarifa kutoka Mahakama kuu kanda ya Mwanza zinaarifu kuwa Familia ya Alphonce Mawazo na Chadema wameshinda kesi dhidi ya Jeshi la Polisi ya kuzuia mwenyekiti huyo wa Chadema Geita asiagwe jijini Mwanza baada ya kuuawa kinyama kwa kukatwa mapanga
Amri ya Jeshi la polisi kuwa Mawazo asiagwe Mwanza kwa kuwa kuna hofu ya kipindupindu imetupiliwa mbali na Mahakama hiyo.
Mahakama
hiyo iliyoketi chini ya Jaji Lameck Mlacha imetoa ruhusa mwili wa
Alphonce Mawazo kuagwa jijini Mwanza na imeagiza Jeshi la Polisi kutoa
Ulinzi siku hiyo lakini Ulinzi huo usivuke mipaka.
Sehemu ya hukumu ya kesi hiyo inasema "Kazi ya Polisi ni kulinda raia na si kuzuia mazishi.."
Mpekuzi blog
CHADEMA YASHINDA KESI YA KUAGA MWILI WA MAWAZO...HUKUMU YAFAFANUA."Kazi ya Polisi ni kulinda raia na si kuzuia mazishi.."
Reviewed by KUSAGANEWS
on
November 26, 2015
Rating:
No comments:
Post a Comment